Our Project
Usafi wa hedhi shuleni.
-Historia ya Mradi
-Mnamo mwaka 2009-10 shirika la maendeleo la Uholanzi
– SNV likishirikiana na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo Water Aid na UNICEF
waliwezesha wizara nne zikiwemo wizara ya elimu,afya, maji na serikali za mitaa katika kuendeleza na
kuongoza miundombinu ya maji, mazingira
na afya kwa kutumia miongozo ya Tanzania kwa njia shirikishi. SNV imekua
ikitekeleza miradi ya afya na maji shuleni
kwa takribani wilaya 9 hapa Tanzania kwa kufuata muongozo wa SWASH
Shirika la SNV kwa kushirikiana na Halmashauri ya (W) Magu,Sengerema, Karatu, Siha, Mufindi, Njombe, Chato na Babati,lilifanya utafiti katika masuala yanayohusiana na kupevuka kwawatoto wa kike mashule ni. Tafiti hiyo ilionesha kuwa wasichanawaliopevuka na wanaotazamia kupevuka hawana taarifa sahihiza kutosha juu ya upevukaji na wanatumia njia duni zakujihifadhi wakiwa katika hedhi. Kipato duni kimechangiakuwepo kwa hali ya matumizi mabaya ya bidhaa za kujihifadhikwa watoto wa kike wakati wa hedhi ambazo zimepelekea kuwepokwa changamoto katika kujihifadhi vizuri, kwa usalama na usafi.Utafiti ulibaini zaidi ya 60% ya wasichana walio katika hedhihawatumii pedi sahihi na salama wanapokuwa katika siku zao.Hali hii imesababisha wasichana wengi kudhalilika hasa paleinapojitokeza pasipo na maandalizi ya kukabiliana nayo.
Hali hii imesababisha utoro mashuleni hasa kwa watoto wa kikekwa muda wa siku 3 hadi 7 kila mwezi. Mazingira hayayamepelekea baadhi ya watoto wa kike wanaosoma katika shule zamsingi ku kosa vipindi vya masomo kwa wastani wa vipindi kati ya240 hadi 560; na kwa wanaosoma katika shule za sekondarihukosa vipindi kwa wastani wa kati ya 180 mpaka 430 kwa kilamwaka wa masomo.
Zaidi ya 70% ya wanafunzi wa kike waliofikia umri wa kupatahedhi wamethibitisha kutokufanya vizuri katika masomo yao nawengine kushindwa kumaliza masomo yao.
Hivyo vijana wa kike wanahitaji elimu ya afya na usafi wa hedhikwa kiasi kikubwa. Utafiti uliofanywa na shirika la SNV katika wilaya hizo kwa kushirikiana na Halmashauri, zinaonesha kuwepoShirika la SNV kwa kushirikiana na Halmashauri ya (W) Magu,Sengerema, Karatu, Siha, Mufindi, Njombe, Chato na Babati,lilifanya utafiti katika masuala yanayohusiana na kupevuka kwawatoto wa kike mashule ni. Tafiti hiyo ilionesha kuwa wasichanawaliopevuka na wanaotazamia kupevuka hawana taarifa sahihi za kutosha juu ya upevukaji na wanatumia njia duni za kujihifadhi wakiwa katika hedhi. Kipato duni kimechangia kuwepo kwa hali ya matumizi mabaya ya bidhaa za kujihifadhi kwa watoto wa kike wakati wa hedhi ambazo zimepelekea kuwepo kwa changamoto katika kujihifadhi vizuri, kwa usalama na usafi. Utafiti ulibaini zaidi ya 60% ya wasichana walio katika hedhi hawatumii pedi sahihi na salama wanapokuwa katika siku zao.
Hali hii imesababisha wasichana wengi kudhalilika hasa pale inapojitokeza pasipo na maandalizi ya kukabiliana nayo.Hali hii imesababisha utoro mashuleni hasa kwa watoto wa kike kwa muda wa siku 3 hadi 7 kila mwezi. Mazingira haya yamepelekea baadhi ya watoto wa kike wanaosoma katika shule za msingi ku kosa vipindi vya masomo kwa wastani wa vipindi kati ya 240 hadi 560; na kwa wanaosoma katika shule za sekondarin hukosa vipindi kwa wastani wa kati ya 180 mpaka 430 kwa kila mwaka wa masomo.
Zaidi ya 70% ya wanafunzi wa kike waliofikia umri wa kupata hedhi wamethibitisha kutokufanya vizuri katika masomo yao na wengine kushindwa kumaliza masomo yao.Hivyo vijana wa kike wanahitaji elimu ya afya na usafi wa hedhi kwa kiasi kikubwa. Utafiti uliofanywa na shirika la SNV katika wilaya hizo kwa kushirikiana na Halmashauri, zinaonesha kuwepo na uhitaji mkubwa wa kujenga uwezo wa kujitambua na kujimudu kiafya, wanapoingia katika hedhi, hasa katika shule za msingi.Hivyo, uelewa mzuri wa afya na usafi wa hedhi utasaidia vijana wa kiume na wa kike, kuwa na maamuzi na mtazamo chanya katikamasuala yote yanayohusiana na afya na usafi wa hedhi.
Katika kutekeleza mradi, Tanzania Cares (TZC) wamekabidhiwa
dhamana ya utekelezaji na usimamizi wa
mradi katika wilaya(Magu).
Lengo
la Mradi
- · Kuongeza matumizi ya pedi za kisasa kwa wanafunzi wa kike kwa shule za vijijini na pembezoni mwaa miji
Malengo Mahususi:-
- Kuongeza namba ya wanafunzi wa kike wanaopata na kutumia pedi za kisasa kirahisi
- Kuongeza uelewa wa masuala juu ya elemu ya hedhi na usafi wa mwili kwa wanafunzi wote (wa kike na wale wa kiume)
- Kuongeza faida ya elimu kwa wanafunzi wasichana na wanafunzi wengine (hususani katika mahudhurio,kumaliza na kiwango cha ufaulu)
- Kuandaa na kutengeneza vipindi vitakavosaidia kuinua na kuboresha masuala ya elimu juu ya masuala ya hedhi na usafi (katika kuratibu, kulinganisha na kuangalia ubora wa vifaa vinavyotupatikana.
Utekelezaji
wa Mradi
- Kutambulisha mradi kwa kamati ya maji na usafi ya wilaya (CWST) kwenye halmashauri pamoja na kuchagua shule zitakaanzo anza kujengewa uwezo
2. Kuwajengea
uwezo Waalimu
wa afya na kamati za shule juu ya ukubwa wa tatizo pamoja na kufikia
maazimio juu ya majukumu yao katika kufanikisha mradi huu katika:-
Hii ilikuwa ni semina ya walimu wa afya shuleni na wajumbe wa bodi na kamati za shule. |
- Kumwelekeza
mzazi kutengeneza mazingira rafiki na binti/kijana
- Kumwandaa
binti katika hali ya kujiamini na kujitunza pindi aingiapo katika hedhi katika
mazingira yoyote (shuleni/nyumbani)
- Kuwashauri
wazazi kuwa mifano halisi juu ya hali ya usafi wa hedhi
- Kutenga
bajeti katika masuala ya hedhi kwa watoto wao kila mwezi
- Kutoa
mapendekezo kwa kuwashirikisha wazazi na wadau wa maendeleo juu ya namna ya
upatikanaji wa pedi shuleni
- Kuvunja
ukimya katika suala zima la hedhi kwa watoto wao.
3. Kuwajengea
uwezo waalimu wakuu na waratibu wa
elimu kata katika shule za msingi
na sekondari.
4. Kuwajengea uwezo madiwani
na kuwashirikisha katika mpango mzima wa uchangiaji gharama
katika upatikanaji na
garama nafuu wa pedi shuleni)
Washiriki
wa utekelezaji mradi
Shirika la maendeleo la Uholanzi - SNV na Tanzania Cares (TZC)
Eneo
la mradi
Wilaya ya Magu, kata za: Nyigogo, Kitongosima,
Kongoro, Nkunguru, Nyanguge, kahamgara, Magu mjini, lutale na Lubugu ambapo
jumla ya shule 21; za msingi zikiwa 11
na za sekondari 10 zimehusishwa.
Maendeleo
ya mradi
Kazi ambazo zimekwisha kufanyika hadi sasa ni:
- Kuutambulisha mradi katika halmashauri husika (Magu)
- Kutembelea shule 21 katika kata 9 kwa ajili ya utambulisho wa mradi
- Makundi ambayo yameshajengewa uwezo katika kata za mradi ni pamoja na:
-Waalimu wa afya na walimu wakuu wa shule
-Kamati na bodi za shule
-Waratibu elimu kata
-Madiwani
-Kamati na bodi za shule
-Waratibu elimu kata
-Madiwani
- Kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wanaohusika moja kwa moja kwenye huu mradi katika ngazi tofauti tofauti (waalimu wakuu na walimu wa afya na malezi katika shule zilizoteuliwa, waratibu elimu kata, wajumbe wa bodi na kamati mbalimbali za shule katika wilaya husika.
Mafanikio
yaliyopatikana katika kazi ambazo zimekwisha kufanyika ni pamoja na:-
Uhamasishaji umefanyika katika ngazi
mbalimbali na kupokelewa vyema kuanzia halmashauri, kata na ngazi ya shule
jambo linaloonesha kuwepo mwanga na mwanzo
mzuri katika kufanikisha mradi.
0 comments:
Post a Comment